Na Jhikoman
Ukombozi wetu upo mikononi mwetu,
Amka binti wa Afrika, Amka mwana wa Afrika
Nyumba yetu inaungua
Nyumba yetu inafuka moshi wa Afrika
Amka mwana wa Afrika Amka
Huo moto nyumba imeshika moto huo moto
Huo moto nyumba imeshika moto huo moto
Nyumba yetu moto imeshika
watu wangu bado wanalala
Si rahisi mimi pekee kuuzima
huu moto mkubwa sana
Nikaite majira wengi wao hayawani
Mabigwa wa kurubuni
Wasije chochea kuni
Vilo vyetu watie kapuni
Waingie navyo mitini
Huo moto nyumba imeshika moto huo moto
Huo moto nyumba imeshika moto huo moto
Wanyumba yetu wazee
Wamelewa hongo wote
Walewe mpaka wabebwe
Ndimi zao ziwe zembe
Midomo isifunguke
Wasije sema chochote
Huo moto nyumba imeshika moto huo moto
Huo moto nyumba imeshika moto huo moto